Nchini Nigeria, kumezinduliwa Mahakama maalum ya kijeshii, itayosikiliza kesi dhidi ya maafisa 36 wa kijeshi, walioshtakiwa kupanga njama za kumpindua rais Bola Tinubu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uzinduzi huu umefanyika siku ya Ijumaa, jijini Abuja ambapo Majaji wa kijeshi watakaosikiliza kesi hiyo, wameapishwa.

Hatua hii inakuja baada ya serikali mwezi Januari kutangaza kuwa, kulikuwa na mpango wa kuipindua serikali mwishoni mwa mwaka uliopita, lakini harakati hizo hazikufanikiwa.

Uzinduzi wa Mahakama hiyo, haioneshwa wazi kwa umma, huku raia sita wa kawaida na Meja Jenerali msaafu wakifunguliwa mashtaka mapema wiki hii kwa kuhusika na mpango huo.

Washukiwa hao ambao wamekanusha mashtaka hayo mbele ya Mahakama ya kiraia, wamedaiwa kuwa walifahamu kuwa Kanali wa jeshi Mohammed Alhassan Ma’aji na wenzake, walipanga mapinduzi hayo, lakini hawakuripoti kwa mamlaka.

Majina ya wanajeshi hao bado hajawekwa wazi, katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye historia ndefu ya mapinduzi ya kijeshi, kabla ya kureja kwa utawala wa kiraia mwaka 1999.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *