
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ametahadharisha kuwa Washington haina uwezo wa kuweka mzingiro wa kijeshi wa majini dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, na kuapa kuwa kushindwa kihistoria wanajeshi wa Marekani huko Tabas na Isfahan kutarudiwa katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Gholam-Hossein Mohsen Ejei ameandika katika akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba kumbukumbu ya fedheha ya wanajeshi wa Marekani huko Tabas sasa imebeba maana tofauti kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Operesheni iliyofeli kwa jina la Eagle Claw ya wanajeshi wa Marekani , mwezi Aprili 1980 ambayo haikufanikisha kuwapata mateka wa Marekani mjini Tehran ilihitimishwa kwa kukabiliwa na dhoruba ya mchanga wa jangwani ambayo iliua askari wanane vamizi.
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema: “Makomando wa adui walioshindwa katika vita vya hivi karibuni walichanganyikiwa huko Isfahan na wamepata kipigo na somo kali kutoka kwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.