Kansela wa Ujerumani ameonya kwamba matokeo mabaya ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran hayaishii kwenye ongezeko la bei ya mafuta, bali pia yanatishia misingi ya uchumi wa Ujerumani.

Shirika la Habari la Mehr limeripoti kuwa, Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz amesema: Mgogoro wa Asia Magharibi unasababisha mshtuko wa kijiopolitiki kwa masoko ya nishati barani Ulaya, Asia na Amerika.

Friedrich Merz ameonya kwamba athari mbaya za vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran haziishii katika ongezeko la bei ya mafuta, bali pia zinatishia misingi ya uchumi wa Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani amesisitiza kuwa athari mbaya za vita hivyo zinaongezeka kila uchao katika usambazaji wa nishati na utulivu wa kiuchumi.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimesababisha hasara kubwa kwa uchumi wa dunia hasa katika sekta za nishati, kilimo na usafirishaji wa baharini, jambo ambalo limepelekea kupanda juu gharama za maisha katika nchi mbalimbali dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *