
Mahakama ya rufaa nchini Kenya imeamua kuwa uavyaji mimba nchini humo, sio haki ya binadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi huu, unabadilisha maamuzi ya Mahakama Kuu mwaka 2022, ambayo iliamua kuwa, utoaji mimba ni haki ya kikatiba na wanaotaka huduma hiyo, wanapaswa kulindwa.
Majaji wa Mahakama ya rufaa, katika uamuzi wao wamesisitiza kuwa uaviaji mimba sio haki ya kikatiba, na Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kupotosha.
Mvutano wa kisheria, ulianza mwaka 2019 baada ya afisa wa afya Salim Mohammed kutoka Kilifi kukamatwa na polisi na kushtakiwa kwa kumtoa mimba msichana mwenye umri wa miaka 16.
Kenya ni taifa ambalo raia wake wengi ni Wakiristo wanaopinga hatua hiyo licha ya katiba kueleza kuwa uavyaji mimba unaweza kufanyika iwapo maisha ya mama mja mzito hapo hatarini.
Hali hii imesababisha maelfu ya wanawake nchini humo kuhatarisha maisha yao kwa kujificha na kutoa mimba.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake nchini humo, yanasema kuwa wanawake saba hupoteza maisha kila siku, wakijaribu kutoa mimba.
Wanaharakati wanasema, wamesikitishwa na uamuzi wa Mahakama ya rufaa na watakataa rufaa kwenye Mahakama ya Juu.