Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mstaafu Mohamed Chande, amesema tume hiyo inataka uwajibikaji wa haki kwa waliohusika na matukio ya vifo vya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 28, 2026, Jaji Chande amesema tume imefanya kazi yake ya uchunguzi na ikatoa mapendekezo kwa kile kilichobainika na kupendekeza kuwa iundwe tume ya kuchunguza makosa ya Jinai na Madai ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

“Kwanza hakuna mtu yeyote aliyekuja mbele ya tume akasema kusiwepo na uwajibikaji, sote tunakubaliana. Si jambo geni kila mmoja tunakubaliana kuwe na uwajibikaji na hakuna aliyesema hapana, kila mmoja ametaka uwajibikaji lakini tunachosema kuwe na uwajibikaji wa haki.

“Tulishauriwa na viongozi wakuu wa nchi tuliowaona kwamba anayestahili kuwajibika awajibishwe kwa mujibu wa sheria na asiyestahili kuwajibishwa asiwajibishwe. Wengine wakaenda mbali zaidi kwamba asitolewe mtu kafara kwenye kuwajibishana. Ushauri huo tulipokea na ilibidi tusikilize pia maoni ya watu,” amesema Jaji Chande.

Amesema hawaamini katika uwajibikaji wa rejareja ambao ni mtu kutiwa hatiani na kuachiwa huru kwa kukosekana ushaidi wenye uzito unaojitosheleza kwa Mahakama kuchukua hatua stahiki.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *