Chombo cha habari cha Kizayuni kimechambua kuporomoka kwa nafasi ya utawala wa Israel duniani na kubadilika fikra za umma kuhusu utawala huo.

Kanali ya 12 ya Israel imetangaza: “Jina “Netanyahu” limekuwa sawa na “shetani” kwa watu wengi duniani.

Kanali hiyo imeongeza kusema: “Ni vigumu kutozingatia kubadilika simamo wa Italia na kuwa dhidi ya “Israel,” ambayo nafasi yake inaporomoka bila mpaka.”

Televisheni hiyo imeongeza kuwa: “Israel inaendelea kuporomoka, sio tu katika majukwaa ya siasa, bali pia mbele ya maoni na fikra za waliowengi na taasisi za kiraia” kote duniani.”

Ripoti hiyo imetolewa siku chache baada ya kutangazwa matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) ambayo yameonyesha kupungua umashuhuri wa Netanyahu kama Waziri Mkuu katika baraza la mawaziri la siku zijazo la utawala wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *