Jeshi la Iran, linasema kuna uwezekano vita kati yake na Marekani huenda vikarejea, na Tehran ipo tayari iwapo Washington itaanza mashambulizi mapya.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mohammad Jafar Asadi, afisa mwandamizi wa jeshi la Iran, amesema ushahidi unaonesha kuwa Marekani haioneshi nia ya kutekeleza ahadi au makubaliano ya kusitsha vita.

Kauli hii ya jeshi la Iran inakuja baada ya rais Donald Trump kusema, Marekani hairidhishwi kabisa na mapendekezo ya Iran kuhusu namna ya kumaliza vita.

Trump ameendelea kusisitiza kuwa, Marekani haiwezi kuruhusu Iran iendelee na mpango wake wa nyuklia.

Wiki iliyopita, kulikuwa na mpango wa kuwepo kwa awamu nyingine ya mazungumzo jijini Islamabad nchini Pakistan, baada ya yale ya kwanza kumalizika bila suluhu.

Nchini Marekani kura za maoni za shirika la IPSOS, iliyochapishwa na vyombo vya Habari vya Washington Post na ABC, asililmia 61 ya raia wa Marekani wanaamini kuwa, rais Trump alikosea kwa kuishambulia Iran kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *