Waathiriwa wa shambulio hilo, lililotokea siku ya Alhamisi, Aprili 30, katika Jimbo la Niger, magharibi mwa Nigeria, walishutumiwa kuwa watoa taarifa kwa kundi la wanajihadi la Ansaru, ambalo liliibuka kutokana na mgawanyiko ndani ya Boko Haram mwaka wa 2021.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Abuja, Moise Gomis

Shambulio hilo lilitokea siku ya Alhamisi, Aprili 30, katika Jimbo la Niger, katikati-magharibi mwa Nigeria: wakifuatana na wanamgambo kutoka nchi jirani ya Benin, wanamgambo wa Nigeria wanaofanya kazi pamoja na jeshi la nchi hiyo waliwaua wafugaji zaidi ya  40 kutoka jamii ya Fulani wanaoshutumiwa kuwa watoa taarifa kwa kundi la wanajihadi la Ansaru, kulingana na vyanzo vya ndani vilivyowasiliana na shirika la habari la AFP.

Kindi hili la Ansaru ambalo lilianzishwa kutokana na mgawanyiko na wanajihadi wa Boko Haram mwaka wa 2021, limejiunga na Al-Qaeda (AQIM) na limekuwa likifanya mashambulizi pande zote mbili za mpaka wa Benin na Nigeria kwa miaka miwili iliyopita.

Kulingana na shirika la habari la AFP, ambalo lilikusanya shuhuda kadhaa, vijana wengi kutoka jamii ya Fulani wanaoshukiwa kuwa watoa taarifa wa Ansaru wamekamatwa, huku wale waliopinga wakiuawa. Jumla ya watu 41 wameuawa, kulingana na Ahmad Ali, kiongozi wa kimila.

Wakati Ali akielezea “operesheni ya pamoja kati ya wanamgambo wa jamii na wale kutoka nchi jirani ya Benin, kwa msaada wa wanajeshi wa Nigeria,” Abdullahi Nasir, mkuu wa serikali katika eneo la Borgu, aliyewasiliana na Idhaa ya Hausa ya RFI, anathibitisha kupelekwa kwa wanamgambo wa Nigeria na anabainisha uwepo wa wanamgambo kutoka Benin  kutokana na ukaribu wa mpaka.

Hata hivyo majeshi ya Nigeria na Benin yamekataa kuzungumzia suala hili.

Chanzo cha kibinadamu kinachotoa msaada kwa jamii zilizohamishwa na vurugu katika eneo hilo kilitoa idadi ndogo ya vifo 38, kikiwashutumu “wanamgambo wa kujilinda kutoka Nigeria na Benin.”

Mkazi wa Kabe amesema kwamba operesheni hiyo ilikuwa “shambulizi la kuzuia” kufuatia vitisho kutoka kwa wafugaji wa Fulani kuvuruga shughuli za kilimo katika eneo hilo, baada ya mauaji ya hivi karibuni ya ndugu zao wawili wanaoshutumiwa kuwa watoa taarifa wa kundi la wanajihadi la Ansaru katika jamii jirani ya Sabalunna.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *