
Nchini Mali, taarifa zinaonyesha kuwa hali ya usalama inazidi kutulia katika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mapigano, wakati wapiganaji wa kijihadi kutoka kundi linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM) na waasi wanaotaka kujitenga kutoka kundi la Azawad Liberation Front (FLA) wakiwa katika mashambulizi tangu Aprili 25 kote nchini, hasa kaskazini, hakuna mapigano yaliyoripotiwa mwishoni mwa wiki.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika mji mkuuu wa Mali, Bamako, kizuizi kilichotangazwa siku ya Jumanne, Aprili 28, na JNIM kimetekelezwa hatua kwa hatua, na kuzuia usafiri na kuwafanya wadau mbalimbali kuchukua hatua kali za tahadhari. Ripoti zimeibuka za mauaji ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kijihadi.
Kaskazini mwa Mali, jiji la Kidal linabaki chini ya udhibiti wa FLA na JNIM, ambazo pia zimedhibiti Tessalit tangu siku ya Ijumaa, Mei 1. Kambi hii imeachwa na jeshi la Mali na kikosi cha wanamgambo wa Urusi cha Africa Corps. Msafara wao kisha ulifika Aguelhok, ambapo dalili za kuondoka pia zilizingatiwa, ingawa mji huo haukuwa umetelekezwa—kinyume na ripoti za awali zilizochapishwa isivyo haki na RFI.
Mashambulizi ya anga na pande hasimu zikidai kuhusika
Huko Timbuktu, Gao, na Ménaka, wakazi wa miji mikubwa katika mikoa ya kaskazini wanajiuliza kuhusu maeneo ynayofuata mashambulizi ya makundi haya yenye silaha, ambayo yanakusudia kuendelea kusonga mbele. Baada ya kukabiliwa na mashambulizi kadhaa huko Gourma Rharous, katika mkoa wa Timbuktu, jeshi la Mali lilifanya mashambulizi ya anga karika eneo hilo mwishoni mwa wiki. Kikosi cha wanamgambo wa Urusi cha Africa Corps, kwa upande wake, kimetoa madai mengi yasiyoweza kuthibitishwa ya wapiganaji wa kijihadi waliouawa katika maeneo ya Ségou, Mopti, na Nara.
Barabara zafungwa, watu wamechomwa moto na kukatwakatwa
Huko Bamako, ambapo JNIM inaendesha harakati zake kwa uhuru bila ya kutegemea FLA, wapiganaji wa kijihadi wanatekeleza kizuizi kilichotangazwa siku ya Jumanne, Aprili 28. Barabara kadhaa zinazounganisha mji mkuu na sehemu nyingine ya nchi zimefungwa. Wakazi waliowasiliana na RFI wameelezea kwamba hawawezi tena kutumia barabara zinazoelekea Kayes, Ségou, na Sikasso, ingawa baadhi ya njia za kupita zilikuwepo. Hakuna kinachokosekana kwa sasa katika mji mkuu, na bei za bidhaa mbalimbali hazipandi, lakini baadhi ya familia zimeanza kuhifadhi chakula kama tahadhari. Siku ya Ijumaa, Mei 1, msafara mkubwa wa meli za mafuta uliweza kuingia katika mji mkuu, chini ya ulinzi wa kijeshi.
Katika siku nane zilizopita, mauaji ya kutisha yaliripotiwa: watu wasio na silaha, wanaoshutumiwa kuwa wapiganaji wa kijihadi—kwa sababu ni kutoka jamii ya Wafulani au wanavaa mavazi ya kimila tu na vilemba—walichomwa moto na kukatwakatwa viungo vyao mchana kweupe. Picha zilizotumwa kwa RFI ni zinahuzunisha. Idadi kamili ya watu waliotendewa ukatili huo haijulikani. Baadhi ya vyanzo vinadai kuwa vimerekodi watu zaidi ya kumi.
Egyptair yafuta safari zake kwenda na kutoka Mali
Uwanja wa ndege wa Bamako unafanya kazi, lakini shirika la ndege la Egyptair lilitangaza siku ya Jumamosi, Mei 2, kwamba limefuta safari zake zote za ndege zilizopangwa kwa ajili ya Hija ya mahujaji kwenda Makka, na kuathiri abiria 4,000, kutokana na “hali ya usalama” na bei za mafuta.
Mountaga Tall, wakili, mwanasiasa, na mwanharakati anayepambana kwa ajili ya demokrasia nchini Mali, alitekwa nyara kutoka nyumbani kwake usiku wa Jumamosi, Mei 2, kuamkia Jumapili, Mei 3, na wanaume wenye silaha na waliojifunika nyuso zao. Mfumo wa huu ni wa vikosi vya usalama vya Mali. Familia yake haijapata habari yoyote kumhusu tangu wakati huo. Katika hatua hii, kutekwa kwake hakujaelezewa rasmi na bado hali hii iko nje ya mchakato wowote wa kisheria.