Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Assimi Goita, amechukua nafasi ya Waziri wa ulinzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wake wa ulinzi, Sadio Camara aliyeuawa katika mashambulizi ya waasi juma moja lililopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo lake limekuja wakati huu Bamako ikikabiliwa na mgogoro wa kiusalama hasa kutokana na mashambulizi ya waasi wa Tuareg wanaoshirikiana na wanajihadi wa Kiislamu dhidi ya ngome za wanajeshi wa Serikali, mashambulio waliyoanzisha wiki moja iliyopita.

Waasi hao walifanikiwa kuchukua mji muhimu wa kaskazini mwa nchi hiyo, Kidal, katika moja ya mashambulio makubwa zaidi kuwahi kufanya na wapiganaji wenye silaha katika kipindi cha karibu miaka 15.

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu takribani 23, huku shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF likiripoti kuwa raia wa kawaida na Watoto ni miongoni mwa waliouawa.

Kupitia tangazo alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Goita amesema amechukua nafasi hiyo kwa lengo la kuhakikisha ulinzi wa raia wa nchi hiyo, akiwataka waliunge mkono jeshi na Serikali yake katika kurejesha udhibiti wa maeneo yaliyochukuliwa na waasi hao.

Aidha Goita amesema naibu wake atakuwa Jenerali Oumar Diarra, ambaye amekuwa akihudumu kama mnadhimu mkuu wa jeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *