Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Nyangasa amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayoendelea wilayani humo hadi Mei 15, 2026.

Akizungumza katika Uwanja wa Ubembeni, Nyangasa amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi wengi wa eneo hilo ni kutokujua pa kuanzia wanapokumbana na matatizo ya kisheria, hali inayochelewesha upatikanaji wa haki.

Amesema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu na msaada wa moja kwa moja kwa wananchi, hususan wasiokuwa na uwezo wa kugharamia huduma za kisheria.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali na Mratibu wa kampeni hiyo wilayani Kondoa, Everitt Magile Steph, amesema migogoro ya ardhi imeonekana kuongoza kwa wingi wa kesi zinazowasilishwa.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *