Wakazi wa Dodoma na wananchi kwa ujumla wametakiwa kuacha dhana potofu na kutumia huduma za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuandika na kutunza wosia ili kulinda mustakabali wa familia zao.
Akizungumza katika Uwanja wa Mtekelezo, katika Halmshauri ya Jiji la Dodoma, Afisa Sheria kutoka RITA, Emmanuela Mwingira amesisitiza kuwa kuandika wosia si uchuro, bali ni mkakati wa kisheria wa kupunguza migogoro ya kifamilia na kuandaa maisha bora kwa warithi pindi mhusika anapotangulia mbele za haki.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)