#HABARI: Zaidi ya wananchi 300 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamefikiwa na kuhudumiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika kipindi cha siku sita tu tangu kuanza kwa awamu ya pili ya Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Kampeni hiyo, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imelenga kusogeza huduma za kisheria na usajili karibu na wananchi ili kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha ya kila siku.
Akizungumza wakati wa Utekelezaji wa kampeni hiyo leo Jumatano, Mei 06, 2026, Afisa Sheria kutoka RITA, Bi. Emmanuela Mwingira amebainisha kuwa mwitikio wa wananchi ni mkubwa, ingawa wengi wanakabiliwa na changamoto ya kukosa viambatanisho muhimu vinavyohitajika katika mchakato wa kupata vyeti vya kuzaliwa.
Bi. Mwingira amesisitiza kuwa cheti cha kuzaliwa ni kielelezo cha msingi kinachofungua milango ya huduma nyingine muhimu kama Bima ya Afya na Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Aidha, amewahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kupata elimu kuhusu uandishi wa wosia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)