Kupitia taarifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na msemaji wake Stéphane Dujarric, Katibu Mkuu amesema anapongeza juhudi za Marekani katika kuwezesha kufikiwa kwa makubaliano hayo na kuunga mkono kikamilifu utekelezaji wake.

“Katibu Mkuu anakaribisha tangazo la usitishaji mapigano kwa siku tatu kuanzia tarehe 9 hadi 11 Mei, pamoja na mpango wa kubadilishana wafungwa kwa kiwango kikubwa kati ya Ukraine na Urusi. Anapongeza juhudi za Marekani katika kuwezesha makubaliano hayo na anaunga mkono kikamilifu utekelezaji wake,” amesema msemaji huyo.

Aidha, Katibu Mkuu amesisitiza tena wito wake wa kuwepo kwa usitishaji wa mapigano wa haraka, kamili, usio na masharti na wa kudumu kama hatua ya kwanza kuelekea amani ya haki, endelevu na ya kina.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wito huo wa Guterres inapaswa kuzingatiwa kwani ni msingi kama ulivyo ainishwa kwenye Hati ya Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa pamoja na maazimio kadhaa yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na Ukraine na Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *