Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema wizara hiyo iko tayari kuwaingiza wabunifu vijana walio katika sekta ya ujenzi kwenye miradi mbalimbali kwa kushirikiana na kampuni za ndani na kimataifa ili kukuza ujuzi wao na Taifa kunufaika nao.
Waziri Ulega ametoa tamko hilo wakati akimkabidhi mwanafunzi aliyeandika wazo bora la kibunifu la mradi wa kutokomeza foleni nchini katika shindano lililoanzishwa na Wizara hiyo na kushirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali sambamba na wabunifu wengine.
Katika shindano hilo mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Tukay Thomas ameibuka mshindi na kuzawadiwa Shilingi Milinoo 10, cheti cha kutambua ushindi wake, ngao na kompyuta mpakato sambamba na fursa ya kufanya kazi na kampuni za ujenzi za ndani.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)