Malipo kwa walimu wanaojitolea katika Kijiji cha Ilekanilo wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza yamegeuka kuwa mzigo kwa wazazi wanaochangishana, ili walimu wanaojitolea wa shule za msingi na sekondari waweze kulipwa.
Wazazi wa kijiji hicho wameiangukia serikali iwaondolee kero hiyo, kwani wanatakiwa kulipa shilingi 500 kila mwezi, huku anayeshindwa kutimiza mchango huo, anaangukia kwenye adhabu ya kutoa mfuko mmoja wa saruji.
Taarifa na Innocent Aloyce.
Mhariri | Abuu Yusuf.
#HabariWikiendi #AzamNews #AzamTVUpdates #Elimu
(Feed generated with FetchRSS)