
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, barabara kati ya Bukavu na Uvira, imefungwa tena kuanzia leo Jumatatu, baada ya kufunguliwa tena mwezi mmoja uliopita. Kwanini hatua hii imechukuliwa ?
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi huu ulitangazwa na Kaimu Gavana wa Kivu Kusini Jean-Jacques Elakano, akieleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.
Aidha, amesema uamuzi huu unakenga kuwaliunda raia wa kawaida dhidi ya mashambulizi yanayoweza kuwalenha katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya serikali na waasi wa M23/AFC.
Amesema hatua hii inalenga pia kuwazuia waasi kutotumia fursa ya kufungiliwa kwa barabara hiyo, kuchukua maenei zaidi.
Kufungwa kwa barabara hii miezi kadhaa iliyopita kulitatiza shughuli za kiuchumi na safari kati ya Bukavu na Uvira, na hatua hii mpya, inatarajiwa kuendeleza hilo, hilo utawala ukisisitiza kuwa ni kwa sababu za kiusalama.