MCHEZO wa Dabi ya Kariakoo katika Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa sare ya 2-2, umeiletea Yanga maumivu makali ikipgwa faini ya Sh30 milioni huku maafisa wake wawili wakikumbana na adhabu za kusimamishwa.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 11, 2026 na Kamati ya Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania, imesema katika mchezo huo wa Mei 3, 2026 dhidi ya Simba, Yanga imepigwa faini ya Sh30 milioni kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Kwenye tukio hilo, Yanga ilitumia nyumba iliyo nje ya uwanja upande wa pili wa barabara kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

YANG 01

Faini hiyo imeweka rekodi kubwa kwa klabu kupewa katika kosa la namna hiyo ambapo kawaida zimekuwa zikitozwa kiasi cha Sh5 milioni hadi Sh10 milioni.

Mbali na faini hiyo, pia Yanga itamkosa meneja wake Walter Harrison aliyesimamishwa kwa mechi tatu kufuatia tukio la kusukumana na kiungo wa Simba, Clatous Chama, huku pia akitozwa faini ya Sh1 milioni.

YANG 02

Shabiki wa Yanga, Mohammed Mposo ambaye amekuwa akiambatana na maafisa wa timu hiyo, naye amefungiwa kwa miezi 12 kwa kosa la kuingia kwenye eneo la kuchezea wakati wa mapumziko siku ya mchezo dhidi ya Simba.

YANG 03

Taarifa hiyo imesema kuwa Mposo kwenye tukio hilo alionekana akimwaga vimiminika ndani ya eneo la kuchezea kitendo  kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *