Angalau watu 72, wengi wao wakiwa raia, waliuawa katika shambulio la anga la jeshi la Nigeria lililolenga soko lililojaa watu katika Jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria, kiongozi wa jamii ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu, Mei 11. Shirika la Amnesty International Nigeria limeripoti kwamba “angalau raia 100” waliuawa, huku mkazi mmoja akisema idadi ya vifo ni 117.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Mamlaka ya Nigeria lazima ichunguze shambulio la anga la kijeshi lililoua raia wasiopungua 100 siku ya Jumapili katika soko la Tumfa, katika Eneo la Serikali ya Mitaa ya Zurmi, Jimbo la Zamfara.” Miili mingine bado inatafutwa, huku waathiriwa wengine wakifariki wakati wakipelekwa hospitalini,” Amnesty International Nigeria ilisema.

Shambulio hilo lilipiga soko la Tumfa siku ya Jumapili katika mji wa Zurmi, kulingana na vyanzo mbalimbali.

Matukio hayo yalitokea Jumapili, Mei 10, 2026, kulingana namnesty International Nigeria: “Karibu saa sita mchana, watu katika soko la kila wiki waliona ndege za kivita zikiruka juu ya eneo hilo. Karibu saa nane mchana, ndege zilirudi na kufnya mashambulizi sokoni.”

“Majeruhi kadhaa kwa sasa wanatibiwa katika Hospitali Kuu za Zurmi na Shinkafi. Mashahidi waliripoti kwamba wengi wa waathiriwa walikuwa wanawake na wasichana,” Amnesty iliongeza, ikibainisha kuwa “tukio kama hilo lilitokea mwezi Aprili huko Jilli, kwenye mpaka kati ya majimbo ya Borno na Yobe, ambapo zaidi ya raia 100 waliuawa na shambulio la anga la kijeshi kwenye soko la kila wiki.”

“Wakazi wa jamii za Kwashabawa, Birane, Kware, Gangara, na Manawa waliathiriwa na shambulio hilo la anga,” alisema Garba Ibrahim Mashema, kiongozi wa jamii katika eneo la utawala la Mashema, ambalo linajumuisha Zurmi, akikuliwa na AFP. “Hadi sasa, tumekusanya miili 72, mingine ikiwa haijulikani kutokana na milipuko hiyo. Waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali katika miji ya Zurmi na Shinkafi,” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *