Meya wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal amesema ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.
Bilal maarufu zaidi kwa jina la usanii wa Bongofleva ‘Shetta’ ametoa kauli hiyo baada ya kukagua miradi ya maendeleo ya robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mombasa–Moshi Bar yenye urefu wa kilomita 0.3, ujenzi wa Kituo cha Polisi Bonyokwa na ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa na matundu 45 ya vyoo shule ya sekondari Bonyokwa pamoja na ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa na matundu 45 ya vyoo katika shule ya sekondari Liwiti.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)