Jeshi la Iran limetangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu tena silaha za Marekani kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz na kuingia katika vituo vya nchi za kanda hii. Limesema kuwa njia hiyo ya kistratejia ya majini sasa iko chini ya udhibiti wa kimkakati wa vikosi vya ulinzi vya Iran.

“Kuanzia sasa na kuendelea, hatutaruhusu silaha za Marekani kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz na kuingia katika vituo mbalimbali vya kanda hii,” amesema Msemaji wa Jeshi la Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Akraminia.

“Nchi yoyote inayotaka kupita kwenye njia hiyo ya majini lazima ifuate utaratibu kwa usimamizi wa vikosi vya ulinzi vya Iran ili kupita bila madhara,” amesema Brigedia Jenerali Akraminia katika shughuli ya Arubaini ya Mkuu wa zamani wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi.

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Akraminia, sehemu ya magharibi ya mlango huo wa baharini iko chini ya uongozi wa Jeshi la Walinzi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), huku sehemu yake mashariki ikisimamiwa na Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *