Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amerusha jiwe gizani akisema mfadhili wa klabu hiyo Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ hana tamaa katika uwekezaji wa uwanja wa klabu hiyo.

Kamwe amesema kama GSM angekuwa na tamaa kwenye umiliki wa uwanja huo angeweza kuhitaji asilimia 80 kwake na 20 kwa klabu hiyo.

Kamwe amesema GSM amekuwa hana maneno mengi ambapo sasa baada ya maneno yake ya Yanga bingwa watamuongezea maneno mengine hana tamaa.

“Unajua kuna wakati unaweza kuwa na tamaa lakini GSM ni tofauti sana hebu angalia anataka asilimia 50 tu lakini ingekuwa mwingine angehitaji hata asilimia 80 ziwe kwake na klabu tubaki na 20,”amesema Kamwe huku akishangiliwa na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

“Sisi Yanga tunakushukuru kwa moyo wako unatupa somo kwamba tuache tamaa kwenye maisha yetu na nadhani GSM amekuwa hataki mambo mengi kuna ile kauli yake ya Yanga bingwa lakini sasa tumuongezee maneno haya hana tamaa.

Yanga imesaini makubaliano na kampuni hiyo kwenye ujenzi wa uwanja huo mpya ambao utajengwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo makao makuu ya klabu hiyo ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *