RAIS wa Yanga injinia Hersi Said amesema mradi wa ujenzi wa uwanja mpya wa klabu hiyo, utawafanya kumiliki asilimia 50 huku mwekezaji akimiliki 50.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini ya mradi huo Hersi amesema, kampuni ya GSM imeonyesha kutotaka tamaa katika umiliki wa uwanja huo kwa kutaka asilimia 50 pekee za umiliki.
Hersi amesema maamuzi hayo yamewapa faraja uongozi wa klabu hiyo, akisema hatua hiyo imeupunguzia mzigo klabu kwa kuwa na nguvu katika mradi huo.
“Wakati tunajadiliana juu ya ujenzi wa uwanja nilishangaa sana kwanini Ghalib Said Mohammed (GSM) haukutumia akili yako ya majadiliano ya umiliki wa mradi,”amesema Hersi.
“Wakati tunajadiliana ukasema unataka kumiliki asilimia 50 pekee za mradi huu hatua ambayo itaifanya klabu yetu nayo kumiliki asilimia 50, hii ni hatua kubwa.”
Aidha Hersi ameongeza kuwa Yanga katika mradi huo mchango wake ni mkubwa ni ardhi wakati GSM ikifanikisha jukumu la uwezeshaji wa kifedha katika kufanikisha uwanja huo.
“Hapa Jangwani tuna eneo lenye ukubwa wa skwea mita 35,000, jukumu letu litakuwa kuwezesha eneo la ujenzi na GSM itafanikisha jukumu la kifedha.