
Mashirika ya Kiislamu nchini Marekani yametangaza kwamba vikao vya Kongresi, ambavyo wabunge wa Republican wametangaza kuwa lengo lake ni kuondoa Sharia nchini Marekani, vimekuwa silaha dhidi ya Waislamu waliowachache kwa kusababisha hofu dhidi ya wafusi wa dini hiiyo.
Baraza la Mashirika ya Kiislamu ya Marekani, ambalo linawakilisha zaidi ya makundi 50 ya Kiislamu, limelaani kutumiwa serikali kama silaha dhidi ya Waislamu wa Marekani” na kusema kwamba vikao vya bunge vinahusika katika kuibia “siasa za hofu.”
Wakati huo huo, Zainab Chaudhry, mkurugenzi wa Baraza la Mahusiano ya Marekani na Kiislamu (CAIR) huko Maryland, amesema: “Vikao vya kupinga Sharia havifanyiki kwa lengo la kulinda Katiba. Vinahusu kuchafua Uislamu na kuwadhihirisha Waislamu wa Marekani kama wageni wa kudumu.”
Jimmy Raskin, kutoka chama cha Democratic na mjumbe mwandamizi katika Kamati ya Mahakama ya Baraza la Wawakilishi, pia amesema kwamba vikao vya kupinga Sharia katika Kongresi ni shambulio dhidi ya uhuru wa kidini.
Wabunge wa chama cha Republican Jumatano iliyopita walifanya kikao mbele ya kamati ndogo ya Mahakama ya Bunge chini ya anwani: “Marekani Bila Sharia: Kwa Nini Uislamu wa Kisiasa na Sheria ya Sharia Haviendani na Katiba ya Marekani.” Kikao kingine kama hicho pia kilifanyika mwezi Februari.
Wakati huo huo Baraza la Mahusiano ya Marekani na Kiislamu (CAIR) linasema lilipokea malalamiko 8,683 ya harakati za kupiga vita Uislamu nchini Marekani mwaka 2025, idadi ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi tangu 1996.