Mamia ya vijana wamejitokeza kushiriki mbio za jogging zilizolenga kuhamasisha amani ya nchi pamoja na kuwaunganisha vijana na f…Mamia ya vijana wamejitokeza kushiriki mbio za jogging zilizolenga kuhamasisha amani ya nchi pamoja na kuwaunganisha vijana na f…

Mamia ya vijana wamejitokeza kushiriki mbio za jogging zilizolenga kuhamasisha amani ya nchi pamoja na kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali za maendeleo.

Akizungumza katika tukio hilo, mwanasiasa na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdul Kambaya amesema vijana wana nafasi kubwa katika kulinda amani ya taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia michezo kama njia ya kuimarisha umoja, mshikamano na afya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Bonanza (KIJA), Gais Mapeo amesema tamasha hilo limeandaliwa mahsusi kuwajenga vijana kijamii na kiuchumi kwa kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na kuwahamasisha kushiriki shughuli halali za kujipatia kipato.

Naye Katibu wa KCC Jogging Kinondoni, Zailuna Othman amesema mwitikio wa vijana umeonesha wazi kuwa jamii ina uhitaji mkubwa wa matukio yanayochochea afya, amani na maendeleo kwa pamoja.

Washiriki wa jogging hiyo walitembea na kukimbia katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni huku wakipeperusha ujumbe wa amani, uzalendo na mshikamano wa vijana katika kuijenga Tanzania yenye maendeleo endelevu

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *