Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kutupa taka hovyo katika fukwe na mifereji ya maji katika maeneo mbalimbali Dar es Salaama, akisisitiza wananchi kulinda mazingira na afya zao kwa ujumla.
Amesema hayo wakati wa zoezi la usafi lililofanyika katika fukwe za Daraja la Salender, jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira.
Mpogolo amepongeza juhudi za taasisi na wadau walioshiriki katika zoezi hilo, akibainisha kuwa kuna umuhimu wa kujenga utamaduni wa kutunza mazingira kila siku ili kuyaacha salama kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Elibariki Bajuta amesema ushirikiano kati ya taasisi na wananchi katika shughuli za usafi wa mazingira ni muhimu katika kuhakikisha maeneo ya pwani na vyanzo vya maji vinaendelea kuwa salama na endelevu.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)
