‘Hatutasalimu amri kamwe’: Pezeshkian aapa kuendeleza mapambano huku Trump akizidi kupiga ngoma za vita‘Hatutasalimu amri kamwe’: Pezeshkian aapa kuendeleza mapambano huku Trump akizidi kupiga ngoma za vita

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameapa kutosalimu amri kamwe mbele ya dola lolote au kutoa kafara heshima ya taifa kwa ajili ya faraja.

Rais Pezehshkian amesema kuwa, baada ya kushindwa kuipigisha magoti Iran katika siku tatu, sasa adui anajaribu kuibua mgawanyiko kati ya watu wa Iran na viongozi wao.

“Hatutasalimu amri. Sitasalimu amri kamwe mbele ya dola lolote. Hatutatoa kafara heshima ya nchi kwa ajili ya kutafuta starehe na tamaa za kidunia, lakini ni lazima tusimamie nchi kwa busara na hekima,” ameongeza Rais Pezeshkian.

Ameeleza kwamba, maadui walimuua shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei bila ya mantiki yoyote ya kisayansi, kisheria au haki za binadamu. Vilevile waliwaua makamanda wa Iran, mawaziri, wanasayansi na wanafunzi wasio na hatia yoyote.

Ameongeza kwamba wale waliodai kutetea haki za binadamu na sheria za kimataifa waliona uhalifu huo lakini walisimama na kutazama tu kwa macho.

“Wanafanya vivyo hivyo kwa kila mtu. Angalia Gaza na Palestina – ni ukatili gani huu wanaofanya!” amekemea Pezeshkian.

Amesema: “Vyombo vya habari vya Marekani vinahalalisha hilo, vikidai kwamba wanajilinda,” na kuongeza kwamba wanaita mauaji ya kimbari kuwa ni kujilinda.

Tarehe 28 Februari, Marekani na Israel zilianzisha vita vya uchochezi dhidi ya Iran kwa kumuua Ayatullah Ali Khamenei na makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa jeshi la Iran katika shambulizi la kushtukiza.

 

Jeshi la Iran lilijibu kwa mawimbi 100 ya mashambulizi yaliyoendelewa kwa siku 40, likilenga taasisi na kambi za kijeshi za Marekani na Israel, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *