Wajibu wa mataifa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa wapitishwaWajibu wa mataifa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa wapitishwa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloimarisha wajibu wa mataifa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, hatua iliyosubiriwa kwa muda mrefu, hata hivyo likipata upinzani mkali toka kwa mataifa wachafuzi wakubwa wa hewa ikiwemo Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo la baraza kuu liliongozwa na kisiwa cha Vanuatu, ambapo awali lilikuwa limeomba maoni ya mahakama ya kimataifa ya haki kuhusu namna mataifa yatawajibika katika kutimiza ahadi zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Maoni yaliyotolewa msimu wa joto na mahakama hiyo yalizidi matarajio ya watetezi wa masuala ya hali ya hewa, mahakama ikitoa uamuzi kwamba ilikuwa “kinyume cha sheria” kwa nchi kupuuza ahadi zao, uamuzi uliofungua mlango wa “fidia” kwa nchi zilizoathiriwa.

Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 141 za nchi wanachama wa baraza kuu la umoja wa Mataifa, huku ni nchi 8 pekee zilipinga ikiwemo Marekani, Urusi na Iran ambao wote hawa ni wazalishaji wakubwa wa mafuta na gesi.

Maoni ya uamuzi wa mahakama ya ICJ ambao hayafungani, yanaruhusu mahakama duniani kote kutumia maoni hayo katika kufanya maamuzi kuhusu kuziwajibisha nchi ambazo zitashindwa kutimiza ahadi zao za mabadiliko ya hali ya hewa.

Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres, amesema huu ni uthibitisho wenye nguvu wa sheria ya kimataifa, haki, sayansi, na jukumu la nchi kuwalinda watu wake kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *