
Nchini Senegali, je, hii ni bahati mbaya ya wakati au mfano mwingine wa mawasiliano yanayokinzana katika ngazi za juu za serikali? Kuanzia Alhamisi, Mei 21 hadi Mei 31, Rais Bassirou Diomaye Faye anapanga kufanya mashauriano na sekta zote za jkiamii katika zoezi la mazungumzo, wakati siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu Ousmane Sonko atahutubia maafisa waliochaguliwa wakati wa kikao cha umma kuhusu masuala ya sasa. Zoezi hili la mawasiliano linaonekana kuwa na uwezekano wa kushindana.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff
Badala ya siku ya mazungumzo ya kila mwaka inayofanyika Mei 28 na mshirika ya kiraia tangu kuanzishwa kwake na Macky Sall mnamo mwaka 2016, Bassirou Diomaye Faye alitangaza nia yake ya kuandaa mashauriano ya siku kumi na makundi mbalimbali ya kijamii, kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa, na viongozi wa kitamaduni na kidini.
“Njia ya kuimarisha taswira yake kama mtu wa mazungumzo,” anaeleza Maurice Soundieck Dione, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Gaston Berger huko Saint-Louis. Ingawa mkuu wa nchi anataka kufanya mashauriano kuwa “mtindo wake wa utawala,” mikutano hii pia inalenga kukabiliana na ukosoaji kutoka kwa vyama vya upinzani, ambavyo vinalaani ukosefu wa mashauriano kuhusu mageuzi ya sheria za uchaguzi, kwa mfano, yaliyopitishwa kwa utata mkubwa, hasa kutokana na tangazo la mfululizo wa mageuzi ya katiba.
Ousmane Sonko kulihutubia Bunge
Wakati huo huo, afisa mwingine wa ngazi ya juu serikalini, Waziri Mkuu Ousmane Sonko, ameahidi kuhutubia Bunge siku ya Ijumaa, Mei 22.
Kikao hiki cha tano cha maswali ya sasa kimepangwa katika kalenda ya Jamhuri, lakini muda wake unaibua maswali. Ili kuepuka mgongano unaoweza kutokea, “uratibu kati ya vikao hivi viwili ungewezekana,” anasema mchambuzi Assane Samb. Lakini katika mpangilio wa sasa wa “ushindani kati ya washirika wapinzani katika ngazi ya juu serikalini” nchini Senegal, muda huu haumshangazi Profesa Maurice Soundieck Dione, kwani kila upande unatafuta “kuwepona kuonyesha nguvu zake. ”
