
Nchini Sudan, zaidi ya vituo 50 vya kutoa lishe katika jimbo la Darfur Magharibi,vimelazimika kusitisha shughuli zao kutokana na kupungua kwa ufadhili, watu karibu laki mbili wakisalia bila msaada.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu misaada, OCHA, limesikitika kuwa tayari hali ya kibinadaam nchini Sudan imekuwa tete na kufungwa kwa vituo hivyo itafanya hali kuwa mbaya zaidi.
Kuna watu zaidi ya milioni nane wanaohitaji msaada wa chakula mwaka huu,wakiwemo watoto milioni tano chini ya umri wa miaka mitano na zaidi ya wanawake milioni tano wajawazito na wale wanaonyonyesha.
OCHA imeonya kuhusu ongezeko la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya raia na miundombinu muhimu ya umma ambayo inazidi kuzuia usafirishwaji wa msaada.
