
Mamlaka nchini Uganda imetangaza kusimamisha usafiri wote wa umma kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo mlipuko mbaya wa Ebola umeendelea kuenea.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Haya yanajiri wakati huu raia wa DRC aliyekuwa akipatiwa matibabu akibainika kutokuwa na maambukizi wakati huu pia wizara ya afya ikitoa mwongozo mpya kwa jamii.
Katibu mkuu katika wizara ya afya Dr Diana Atwine amethbitisha hali ya mwanamke huyo raia wa DRC abaye alikuwa mmoja wa kesi mbili ya wagonjwa wa Ebola mwengine akiwa mwanaume aliye fariki jumma iliyo pita
“Kwa kweli yule aliyekuwa na Ebola, ambaye tunamtunza, anaimarika na amepimwa ambapo amepatikana hana. Kwa hivyo hatuna Ebola nchini. Mara tu atakapopata nguvu, tutamruhusu kuondoka hospitalini” Alisema Diana Atwine, Katibu mkuu katika wizara ya afya.
Pamoja na habari hiyo njema, Serikali imetangaza hatua mpya kadhaa ikiwa ni kupiga marufuku safari zote za ndege kwenda nakutoka DRC,wasafiri wanaotumia mabasi kutoka DRC kwa muda wa wiki nne.
Serikali pia imeziagiza mamlaka katika wilaya zilizo karibu na DRC kutoa taarifa za vifo vyovyote kabla ya kuzikwa ili wataalam wa afya waweze kubaini chanzo cha vifo hivyo.Vikosi vya usalama pia vimeagizwa kufunga masoko yote kwenye wilaya mpakani na DRC.
Rais Yoweri Museveni ametoa wito wa utulivu na kusisitiza kwamba mamlaka nchini Uganda na DRC inapaswa kuzingatia kutambua kesi yoyote haraka na kusimamia matibabu.
“Ebola huenea kwa mawasiliano ya karibu hivyo acha kupeana mikono. Ukiripoti Ebola mapema inatibika. Madaktari wanaweza kudhibiti homa, kutapika na kadhalika, lakini tu ikiwa itaripotiwa kwa wakati. Kwa hivyo mtu aliyeambukizwa anaweza kutibiwa” Alitangza Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Serikali ya Uganda imesisitiza kuwa haijasajili maambukizo yoyote ya Ebola kwenye wanainchi wa Uganda. Lakini imekaza hatua hasa katika mpaka wa DRC na maeneo yenye shughuli nyingi ili kuzuia maambukizi.
Kenneth Lukwago, Kampala, RFI Kiswahili
