
Rais wa Marekani
Donald Trump anasema makubaliano ya kumaliza vita vya Iran “yamejadiliwa
kwa kiasi kikubwa” na maelezo yatatangazwa hivi karibuni.
Katika chapisho kwenye
mtandao wake wa kijamii wa Truth Socialsiku ya Jumamosi, Trump alisema makubaliano hayo yatajumuisha kufunguliwa
tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
Asubuhi ya leo,
shirika la habari la Iran la Tasnim limesema kuwa Mlango wa Bahari utarejea
katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30, na kuongeza kuwa makubaliano
huenda yakasimamisha mashambulizi pande zote.
Muda mfupi ujao tunatarajia
tamko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kufuatia
mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa India mjini New Delhi – unaweza kufuatilia
moja kwa moja hapo juu pindi atakapoanza.
Msemaji wa wizara
ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei aliambia televisheni ya taifa jana kuwa wawakilishi
wa Marekani na Iran wamekuwa wakikutana katika wiki za hivi karibuni.
Lakini alionya hilol
haimaanishi kuwa makubaliano yatafikiwa katika masuala muhimu na kuwashutumu
Wamarekani kwa kutoa “taarifa zinazokinzana”.
Trump pia alisema
alikuwa na “mazungumzo mazuri” na viongozi wa Saudi Arabia, Umoja wa
Falme za Kiarabu, Qatar, na wengine kuhusu “Mkataba wa Maelewano unaohusu
AMANI”.
