Je, kupunguzwa kwa bajeti ya Marekani kumesababisha kuenea kwa mlipuko wa virusi vya EbolaJe, kupunguzwa kwa bajeti ya Marekani kumesababisha kuenea kwa mlipuko wa virusi vya Ebola

Zaidi ya watu 900 sasa wanashukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, nchini DRC kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa jana na Shorka la Afya Duniani, WHO. Shirika la afya la Umoja wa Afrika linasema kwamba zaidi ya dola milioni 300 zinahitajika ili kukidhi mahitaji yanayohusiana na mlipuko huu. Mojawapo ya mashirika yanayobobea katika usaidizi wa kibinadamu linaonekana wazi kwa kutokuwepo kwake leo: shirika la Marekani la USAID, lililovunjwa na Donald Trump mwanzoni mwa muhula wake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeremy Konyndyk, mmoja wa viongozi wa zamani wa USAID, anasikitishwa kupotea kwa utaalamu wa miaka mingi katika kudhibiti aina hii ya mlipuko. Anabaini kwamba bila kupunguzwa kwa bajeti, uamuzi uliochukuliwa na serikali ya Marekani, mlipuko huu mpya wa Ebola ungeweza kugunduliwa mapema zaidi. Na ana matumaini makubwa, amesema alipokuwa akimwambia mwandishi wetu huko Marekani, Vincent Souriau. Mlipuko wa sasa wa Ebola unamkumbusha ule aliopambana nao na timu za USAID katikati ya miaka ya 2010.

“Bila shaka huu ndio mlipuko wa Ebola unaoti wasiwasi zaidi ambao nimewahi kuona,” anasema. “Ningeiweka sawa na mlipuko mkubwa wa mwaka 2014 huko Afrika Magharibi kwa upande wa hatari ya kiafya.” Wakati huo, aliongoza timu za kukabiliana na dharura za USAID, ambazo zilitoa zaidi ya dola bilioni moja kupambana na ugonjwa huo. Na Jeremy Konyndyk ana uhakika na hili. Leo, kama utawala wa Trump haungevunja shirika hili, janga hilo nchini DRC lingeweza kugunduliwa mapema.

Ni bora kufika katika maeneo yaliyoathiriwa

Jeremy Konyndyk pia anapuuzia mbali matangazo ya hivi karibuni kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikiahidi kufadhili – kupitia Umoja wa Mataifa – kliniki hamsini zinazopambana dhidi ya Ebola nchini DRC na Uganda. Ikulu ya White House, anasema, “haina wazo lolote kuhusu matatizo yanayosababishwa na hali hiyo.” Na haitakuwa na msaada wowote bila kufika katika maeneo yaliyoathiriwa kufahamu kwa unadani mlipuko huo na jinsi ya kukabiliana nao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *