
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amependekeza kwa uangalifu kwamba Washington inaweza kuwa na habari njema leo Jumatatu kuhusu uwezekano wa makubaliano na Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tulidhani tunaweza kuwa na habari nzuri jana usiku, labda leo (Jumatatu) inawezekana, nisisemi mengi,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameema kutoka New Delhi, akimaanisha uwezekano wa makubaliano.
Majadiliano kwa ajili ya kufikia makubaliano kati ya Marekani na Iran yanaendelea, huku Donald Trump akiwataka wapatanishi siku ya Jumapili “wasiharakishe mambo.”
Iran inataja maendeleo katika mambo mengi na Marekani, lakini makubaliano hayajafikiwa
Wakati huo huo Iran siku ya Jumatatu imetaja maendeleo katika mazungumzo na Marekani ili kufikia makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita, huku ikifutilia mbali wazo la makubaliano yanayokaribia.
“Ni kweli kusema kwamba tumefikia makubaliano kuhusu sehemu kubwa ya masuala yanayojadiliwa,” amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Esmail Baghai wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kila wiki. “Lakini kusema kwamba kusainiwa kwa makubaliano kumekaribia, hakuna mtu anayeweza kudai hivyo,” ameongeza, akiishutumu Washington kwa kutokuwa na ukweli.
Baada ya wiki kadhaa za vitisho na mazungumzo, Marekani na Iran zinaonekana kuwa karibu kufikia makubaliano ambayo yatamaliza vita vya Mashariki ya Kati ambavyo vimeua maelfu ya watu na kutikisa uchumi wa dunia. Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump amesela hana matumaini ya makubaliano yaliyo karibu siku ya Jumapili, akisema hataki “kuharakisha mambo.”
Siku iliyotangulia, rais wa Marekani alitaja makubaliano “yaliyojadiliwa kwa upana” ambayo yangeruhusu kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
