
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema leo Jumatatu kwamba Israel “daima” itakuwa na haki ya kujilinda bila kujali makubaliano yoyote kati ya Washington na Tehran, akirudia maneno yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Jumatatu, Mei 25, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema kwamba Israeli “daima ina haki ya kujilinda” iwapo kutatokea shambulio kutoka kwa Hezbollah ya Lebanon. Waziri Mkuu wa Israel alisema siku ya Jumapili kwamba Donald Trump alikuwa amesisitiza “haki” ya Israel ya kupigana nchni Lebanon.
Siku ya Jumapili Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kwamba Donald Trump, wakati wa mazungumzo ya simu, alisisitiza “haki” ya Israel ya kupigana nchini Lebanon, ambapo jeshi la Israel linalenga Hezbollah inayounga mkono Iran.
“Israeli daima ina haki ya kujilinda. Kila nchi duniani ina haki hiyo.” “Kwa hivyo, ikiwa Hezbollah inajiandaa kurusha makombora au kurusha makombora dhidi yake, Israel ina haki ya kulipiza kisasi,” Marco Rubio amewaambia waandishi wa habari kutoka New Delhi, ambapo kwa sasa anazuru.
Makubaliano na Iran bado yanawezekana Jumatatu, asema Marco Rubio
Wakati huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amependekeza kwa uangalifu kwamba Washington inaweza kuwa na habari njema leo Jumatatu kuhusu uwezekano wa makubaliano na Iran.
“Tulidhani tunaweza kuwa na habari nzuri jana usiku, labda leo (Jumatatu) inawezekana, nisisemi mengi,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameema kutoka New Delhi, akimaanisha uwezekano wa makubaliano.
