
Mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli Suzana Magufuli, amefariki dunia leo Mei 25, 2026 nyumbani kwake Chato mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli, leo Jumatatu Mei 25, 2026 akizungumza na AyoTV.
Jesca amesema Suzana Magufuli amefariki saa 1:00 usiku akiwa nyumbani kwake Chato.
“Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja usiku nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taratibu za msiba familia itawajulisha. Bwana ametoa na Bwana ametwaa,” amesema Jesca.
Hayati Suzana Magufuli alikuwa akifahamika kama mlezi na nguzo muhimu ya familia ya Hayati Dk Magufuli, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2021.
