Wanne wafariki dunia baada ya treni kugonga basi la shule UbelgijiWanne wafariki dunia baada ya treni kugonga basi la shule Ubelgiji

Watu wanne wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia baada ya treni kugonga basi la shule katika eneo la Buggenhout nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Maxime Prévot amesema ajali hiyo imetokea leo Jumanne Mei 26, 2026 na kusababisha vifo vya watu hao wanne huku wengine wakipata mshtuko mkubwa kutokana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa mamlaka za eneo la Buggenhout kaskazini mwa nchi hiyo, ajali hiyo imetokea saa mbili asubuhi kwa saa za huko.

Waziri wa Sheria wa Ubelgiji, Annelies Verlinden amesema kupitia mtandao wa X kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la shule kugonga treni.

Picha kutoka eneo la tukio zilizochapishwa katika tovuti ya CNN zimeonyesha basi dogo la shule likiwa limeanguka pembeni mwa reli baada ya kugonga treni.

“Maneno yananishinda kuelezea ajali ya Buggenhout iliyohusisha treni na basi la shule,” amesema Verlinden.

Rais wa European Commission, Ursula von der Leyen amesema amehuzunishwa na tukio hilo.

“Nimevunjika moyo kusikia kuhusu ajali hii. Salamu za rambirambi ziende kwa familia za waliopoteza wapendwa wao pamoja na ndugu zao,” amesema kupitia mtandao wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *