
Shirika la kmataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limeituhumu nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE, kwa kuwezesha usajili na mafunzo ya mamluki wa Colombia ili kuwasaidia wapiganaji wa RSF ambao wanatuhumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari nchini Sudan.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti ya hivi punde ya HRW imeelezea namna wanajeshi wa zamani wa Colombia walivyosajiliwa na kampuni binafsi zinazohusishwa na watu walio karibu na serikali ya Emirati, na kisha baadaye kuishia wakipigana sambamba na wapiganaji wa RSF nchini Sudan.
Kulingana na HRW, mamluki hao wa Colombia walikuwepo wakati wa makabiliano mabaya hasa wakati miji ya Darfur na El-fasher zilipoanguka mikononi mwa wapiganaji wa RSF.
Vilevile HRW inasema kuna ushahidi wa mamluki hao kushiriki katika matumizi ya silaha nzito na droni lakini pia utoaji wa mafunzo ya kijeshi kwa watoto.
Wanajeshi wa zamani wa Colombia walio na uzoefu kwenye uwanja wa mapambano kufuatia vita vya miongo sita nchini mwao, mara kwa mara husajiliwa kushiriki katika vita vya kigeni.
Uchunguzi wa AFP mwezi Disemba, ulifichua mpango wa usajili, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa kampuni ya Falme za Kiarabu ya Global Security Services Group (GSSG) pamoja na makampuni mengi nchini Colombia na Panama.
