#HABARI: Ukosefu wa kipato katika baadhi ya familia umeendelea kuathiri elimu ya watoto wa kike katika shule za Jiji la Dar es S…#HABARI: Ukosefu wa kipato katika baadhi ya familia umeendelea kuathiri elimu ya watoto wa kike katika shule za Jiji la Dar es S…

#HABARI: Ukosefu wa kipato katika baadhi ya familia umeendelea kuathiri elimu ya watoto wa kike katika shule za Jiji la Dar es Salaam, ambapo baadhi ya wanafunzi hushindwa kumudu gharama za kununua taulo za kike na hivyo kukosa na hata kutohudhuria masomo kikamilifu wakati wa hedhi, hali inayopunguza ufanisi wao kitaaluma.

Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa taulo za kike katika Shule ya Sekondari Kibasila, Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Nuru Kassian, amesema mpango huo unalenga kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike na kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kujifunzia bila vikwazo na kwamba mpango huo utazifikia shule zote zilizopo ndani ya Manispaa hiyo.

Kwa upande wao, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Dkt. Juma Lenda, pamoja na Fatma Murtaza, wamesema kuwa jumla ya taulo za kike elfu tatu zimepokelewa na zitasaidia wanafunzi kushiriki masomo yao kikamilifu katika mazingira safi, salama na yenye kuzingatia afya zao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *