Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea kutumia maonesho ya biashara kama njia ya kuwatafutia wazalishaji na wajasiriamali masoko mapya ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi huku ikijiandaa kunufaika na fursa za Soko Huru la Afrika (AfCFTA).

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Zanzibar ndani ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema ushiriki wa Zanzibar katika maonesho ya biashara umeendelea kusaidia kutangaza bidhaa zinazozalishwa visiwani pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji.

Mahmoud amesema ushindani katika masoko ya sasa unahitaji wazalishaji kuzingatia ubora wa bidhaa, matumizi ya vifungashio vya kisasa pamoja na utoaji wa huduma bora ili kuongeza uwezo wa bidhaa za Zanzibar kushindana katika soko la Afrika Mashariki na masoko mengine ya kimataifa.

Alisema pamoja na Zanzibar kuwa na eneo dogo kijiografia, visiwa hivyo vina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa na huduma zenye ushindani, huku uwekezaji katika rasilimali watu, ubunifu na matumizi ya teknolojia ukiendelea kufungua fursa mpya za biashara na ajira kwa wananchi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *