Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesema mbali na kuwajengea vijana ukakamavu na uzalendo, jeshi hilo linaendelea kuwalea katika misingi ya nidhamu, kuwapatia mafunzo ya awali ya kijeshi pamoja na kuwapa ujuzi wa stadi mbalimbali za kazi.

Akizungumza baada ya kutembelea banda la JKT katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (Sabasaba), Brigedia Jenerali Mabena amesema vijana hao pia wanapatiwa elimu ya ujasiriamali inayowawezesha kuzalisha na kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya taifa.

Mhariri | @rajjmsangi

#AzamTvUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *