WCF KUWAFIKIA WAFANYAKAZI SEKTA ISIYO RASMIWCF KUWAFIKIA WAFANYAKAZI SEKTA ISIYO RASMI

WCF KUWAFIKIA WAFANYAKAZI SEKTA ISIYO RASMI

#HABARI: Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeeleza kuwa uko katika mchakato wa kuandaa mpango na mazingira wezeshi yatakayowezesha Watanzania wanaojiajiri katika sekta isiyo rasmi kunufaika na huduma za fidia na kinga dhidi ya majanga yatokanayo na kazi.

Hatua hiyo imebainishwa jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya WCF na Chama cha Waandishi wa Habari Wanaofanya Kazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), kilicholenga kutoa elimu kuhusu haki na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa wafanyakazi.

Afisa Matekelezo wa WCF, Ayoub Bendera, amesema mfuko huo unatambua mazingira hatarishi wanayokumbana nayo makundi ya sekta isiyo rasmi kama vile wachimbaji wadogo na mafundi, hivyo mpango huo unalenga kupunguza athari wanazokutana nazo wanapoumia, kuugua, au kupoteza maisha.

Bendera amefafanua kuwa kwa sasa huduma za WCF zinanufaisha zaidi wafanyakazi wa sekta rasmi za umma na binafsi, lakini wanatazama namna bora ya kuwasaidia na wale walio nje ya mfumo huo kwa manufaa ya familia zao.

Wakati wa kikao hicho, Afisa Madai wa WCF alieleza kuwa mfanyakazi aliyesajiliwa hupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu, vipimo, dawa, upasuaji, na vifaa tiba vinapohitajika.

Kufuatia mafao hayo, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Comrade Tumaini Nyamhokya, amewataka wanahabari kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa mifuko hiyo ya hifadhi, akisisitiza kuwa WCF imekuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wanaokabiliwa na changamoto kazini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *