
Kushindwa Trump na Netanyahu katika kufikia malengo yao ya kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi tisa, ni moja ya mada muhimu zinazojadiliwa na taasisi za utafiti, wananadharia mashuhuri na vyombo tajika vya habari.
Katika ripoti yake ya kitafiti ya hivi karibuni, Taasisi ya Baraza la Atlantiki imeseme: “Donald Trump” aliishambulia Iran si kwa msingi wa stratijia bali kwa sababu za kibinafsi, na sasa anatafuta njia ya kujinasua kwenye kinamasi alichokianzisha mwenyewe, ambapo katika upande wa pili Tehran inadhibiti kikamilifu Lango-Bahari la Hormuz kuliko wakati mwingie wowote. Maneno haya ya Baraza la Atlantiki yanaibainishia Washington ukweli mchungu zaidi wa kumalizika vita vya Iran na Marekani. Vita vilivyoanza Februari 2026 kwa ahadi ya kuupindua mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini baada ya miezi mitatu, vinamalizika kwa aibu kubwa zaidi inayoweza kutokea dhidi ya Ikulu ya Marekani.
David Jeffrey Frum, mwandishi wa ripoti hii na afisa wa zamani katika utawala wa George W. Bush, amechunguza kwa makini tabia za Donald Trump ili kuelewa ni kwa nini mtu huyo anayedai kuwa mwerevu kupita kiasi amesababisha kushindwa kukubwa zaidi kimkakati kwa Marekani tangu vita vya Vietnam. Frum anaamini kwamba vita vya Februari 28 havikuwahi kuanzishwa kwa msingi wa mahesabu ya kimantiki, bali vilitokana na kasoro za kimuundo katika tabia za rais wa Marekani; dosari ambazo zinaanzia kwenye uroho na ukosefu wa mpangilio hadi kushawishika haraka na kutokuwa na uwezo wa kuongoza. Kwa maoni yake, Trump alidhani kwamba uamuzi ambao ulikuwa mgumu kwa wengine ungekuwa rahisi kwake.
Haaretz, gazeti la Kizayuni linalochapishwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, pia limekiri kuhusu maafa haya kwa mtazamo wa Tel Aviv na kuandika katika uchambuzi sawa na huo katika kumkosoa vikali Benjamin Netanyahu kwamba: “Ahadi ya ‘ushindi kamili’ imekuwa udhalilishaji wa kimkakati.” Kwa mujibu wa ripoti hii, Netanyahu alidhani kwamba kwa kuishirikisha Marekani katika vita vya pande zote, angeweza kuokoa mustakabali wake dhaifu wa kisiasa, lakini kivitendo, mkondo wa mazungumzo unasonga mbele kwa namna ambayo imeifanya Iran kuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko huko nyuma na kuusukuma utawala bandia wa Israel pembeni mwa maamuzi muhimu.
Mwandishi wa Baraza la Atlantiki anaorodhesha dosari tatu kuu katika tabia ya Trump ambazo zimebadilisha kabisa mkondo wa vita. Kwanza ni kwamba, Trump ni “jasiri asiyechukua tahadhari, asiyetabirika wala kuwa na mpango,” kama alivyofanya katika ghasia za Januari 6, 2021, ambapo alituma wafuasi wake waibue vurugu katika Congress bila kuwa na mpangilio wowote madhubuti. Pili, ni “mlaghai na tapeli anayeshawishika haraka,” sawa kabisa kama alivyosema Marco Rubio, waziri wake wa mambo ya nje mwaka 2016. Trump alitaka Iran “ijisalimishe bila masharti” lakini sasa anatia saini makubaliano ambayo yanaipa Tehran udhibiti mkubwa zaidi wa Lango-Bahari la Hormuz. Kasoro yake ya tatu, lakini ambayo huenda ni muhimu zaidi ni kwamba: Trump “sio kiongozi.” Mtindo wake wa utawala unategemea “kuamrisha,” na sio kushawishi au kuelekeza maoni ya umma.
Gazeti la The New York Times limenukuu tathmini iliyofanywa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na kuandika: ‘Licha ya mashambulizi hayo makali, Iran imerejesha uwezo wake wa kijeshi katika vituo vyake 30 kati ya 33 vya makombora vilivyo kando ya Lango-Bahari la Hormuz na kuendelea kumiliki asilimia 70 ya silaha zake za makombora ilizokuwanazo kabla ya vita. Hii ina maana kwamba Iran imedumisha mpango wake wa amani wa nyuklia na kugeuza vita kuwa fursa ya kuimarisha nafasi yake ya kijiopolitiki katika eneo.’ Gazeti la Haaretz pia limeandika katika tathmini yake kwamba malengo yaliyotangazwa rasmi na Netanyahu, ikiwa ni pamoja na kuharibu mpango wa nyuklia wa Iran, kudhoofisha kabisa Hamas, na kuipokonya silaha Hizbollah, hayajafikiwa.
Trump na Netanyahu sasa wanajaribu kuhadaa fikra za waliowengi duniani kwamba kushindwa huku kwa hakika ni ushindi mkubwa kwao. Frum anaelezea hali hii ya mwisho katika ripoti yake kuwa ya kushangaza: ‘Trump anajaribu kujikinaisha kuwa ameshinda vita, lakini hivi karibuni atatambua kwamba hakuna mtu anayemwamini.’ Baraza la Atlantiki, linasema kuwa somo la msingi linalotokana na vita hivi ni kwamba: ‘Zama za vita vya kawaida vya kuzitwisha nchi nyingine matakwa ya madola makubwa zimepitwa na wakati.’
Katika zama hizi tata za kijiopolitiki, mapambano na kusimama kidete mataifa na nafasi yazo ya kijiopoliti ni silaha yenye nguvu zaidi kuliko ndege za kivita za kisasa. Iran imethibitisha kuwa wanadiplomasia wake, sawa na wanajeshi wake katika mitambo ya kuvurumisha makombora, wana nia thabiti ya kutetea na kulinda maslahi ya taifa na usalama wa nchi yao. Hasa upande wa pili unapokuwa unakabiliwa na tatizo na kuongozwa na mtu ambaye hana uwezo wa kupanga mipango ya muda mrefu. Huenda huu ukawa ukweli mchungu zaidi kwa maadui wa Iran, ambao wachambuzi wengi wa nchi za Magharibi katika tasisi za kifikra sasa wanaukiri hadharani.
