Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inashikilia magari 32 yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria bila kufuata taratibu za kiforodh…Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inashikilia magari 32 yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria bila kufuata taratibu za kiforodh…

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inashikilia magari 32 yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria bila kufuata taratibu za kiforodha ambayo yameikosesha Serikali mapato na kuisababishia hasara Mamlaka hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Upelelezi Dar es Salaam II Omari Kogoda amesema magari hayo yamezuiwa baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kisayansi pamoja na uhakiki wa mifumo ya ndani uliobaini kuwa baadhi ya wamiliki walishindwa kulipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.

Amesema uchunguzi uliofanywa umebaini kuwapo kwa udanganyifu mbalimbali ikiwamo kubadilisha namba za chesisi na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu magari hayo ili kupata punguzo la kodi ambalo hawakuwa na sifa ya kulipata.

Amewataka wananchi ambao magari yao bado hayajafikiwa na ukaguzi kufika katika ofisi za TRA kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya kodi na kumaliza taratibu za umiliki halali wa magari yao.

Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali wametaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wanaokwepa kodi wakidai kitendo hicho kinaikosesha serikali mapato muhimu ya maendeleo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *