Iran yalaani ukiukaji wa Marekani wa makubaliano ya amani, yahimiza UN kuingilia katiIran yalaani ukiukaji wa Marekani wa makubaliano ya amani, yahimiza UN kuingilia kati

Iran imelaani vikali vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamisha vita haramu vya hivi karibun, ikiuhimiza Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baqaei, amesema shambulizi la kijeshi la Marekani dhidi ya maeneo ya mji wa Bandar Abbas, kusini mwa nchi, siku ya Alhamisi, linakiuka ardhi na mamlaka ya kujitawala ya Iran, jambo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linawajibika kutimiza wajibu wake wa kisheria wa kumuwajibisha mvamiz, Marekani,” ameongeza Baqaei.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ameashiria jinsi Marekani inavyoendelea kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran, hasa mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara katika eneo la Ghuba ya Uajemi na bahari kuu, pamoja na mashambulizi ya anga katika maeneo ya kusini mwa nchi katika siku chache zilizopita.

Amesisitiza azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuchukua hatua zote muhimu ili kulinda mamlaka yake ya kitaifa na ardhi yake kwa mujibu wa Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limejibu uchokozi huo kwa kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kambi ya Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Wakati huo huo, Baqaei amelaani matamshi ya vitisho ya maafisa wa serikali ya Marekani dhidi ya Iran na baadhi ya nchi zingine za kikanda, akielezea mshikamano Jamhuri ya Kiislamu na nchi rafiki na ya ndugu ya Oman.

Siku ya Jumatano, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema “atailipua” Oman ikiwa itakubali kufanya kazi na Iran ili kushiriki udhibiti wa Mlango-Bahari wa Hormuz.

“Kutishia ‘kulipua’ nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, ambayo imekuwa na nafasi ya kujenga, yenye ufanisi, na ya uwajibikaji katika amani na usalama wa kikanda, ikitumika miaka mingi kama mpatanishi katika michakato ya kidiplomasia, na kufanya juhudi za kutumikia amani na utulivu wa kikanda, sio tu kwamba kunakiuka kanuni inayokataza vitisho au matumizi ya nguvu, lakini pia ni ishara nyingine hatari ya kuhalalisha uvunjaji wa sheria na uonevu katika mahusiano ya kimataifa,” amesisitiza Baqaei.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *