Chanzo cha picha, Analadu via Getty Images
Zaidi ya watu 400 wamekamatwa kote nchini Ufaransa kufuatia ushindi wa Paris Saint-Germain (PSG) kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal usiku wa jana huko Budapast, Hungary.
Maelfu ya maafisa walitumwa kudhiditi machafuko yaliyotatiza huduma za mabasi, treni na reli katika mji mkuu Paris.
Polisi walirusha vitoa machozi kutawanya umati wa watu katikati mwa jiji huku baadhi yao wakijeruhiwa katika vurumai hilo
Video zilizonaswa jijini Paris na kusambazwa mitandaoni zinaonyesha
miali ya moto ikizimwa, baiskeli zikiwaka barabarani na waltu waliokuwa wapiga kelele wakivunja vioo mbele
ya duka moja.
Eneo maarufu la Champs-Élysées
lilifurika na mashabiki muda mfupi baada ya timu ya Ufaransa kuinyuka Arsenal
kupitia mikwaju ya penalti. Mapema Jumamosi kulikuwa na makabiliano kati ya
polisi na mashabikii waliojitokeza kutazama fainali kwenye skrini kubwa katika
uwanja wa PSG wa Parc des Princes.
Polisi wanasema
magari sita, biashara kadhaa na maeneo la kuegesha mabasi yaliharibiwa wakati
wa machafuko hayo..
Vurugu sawa na hizo zilishuhudiwa wakati PSG iliposhinda kombe hilo mwaka jana, ambapo sherehe za ushindi ziligeuka kuwa machafuko.
Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nuñez amasema mwaka huu, mamlaka ilikuwa imejiandaa vilivyo kudhibiti tukio kama hili likijitokweza.