
Rais wa Madagascar Kanali Michaël Randrianirina, amelihutubi taifa, akizungumza kwa muda mrefu kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumapili jioni, Mei 31, 2026. Hotuba ambayo wengi waliisubiri kwa hamu, ilikuja siku tatu kabla ya uzinduzi wa mashauriano ya kitaifa na wakati ambapo serikali yake inakabiliwa na sintofahamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Madagascar, Aurélie Kouman
Hii ni hotuba yake kuu ya pili tangu aingie madarakani mwezi Oktoba mwaka uliyopita. Mkuu wa nchi alitumia hotuba hiyo kutetea rekodi ya miezi saba ya “Ujenzi mpya,” akiangazia miradi kadhaa inayoendelea: upatikanaji wa maji, umeme, na mageuzi katika elimu ya juu.
Lakini Michaël Randrianirina pia alikiri mapungufu katika kazi yake. Kuhusu ufisadi, alikiri kwamba hakuna kilichobadilika kweli. Neno zito kutamka, ikizingatiwa kwamba mapambano dhidi ya ubadhirifu yalikuwa moja ya ahadi muhimu za maandamano ya vuguvugu la vijana wa GEN Z mnamo mwezi Oktoba 2025.
Makanisa katika mchakato wa mashauriano
Kuhusu mashauriano ya kitaifa, ambayo yataanza Juni 3, amebainisha kwamba yatachukua fomu ya mkutano kati yake, Waziri Mkuu, Waziri anayehusika na Ujenzi mpya, na wakuu wanne wa makanisa ya Kikristo. Tangazo hili lilikuja kama mshangao, kwani Baraza la Makanisa Ulimwenguni lilishutumu kutengwa kwake katika mchakato huo mwishoni mwa mwezi Aprili.
Hatimaye, kuhusu uhusiano wa karibu na Urusi, rais alitetea msimamo wake wa kutokuwa na upande wowote anaoegemea. Alisisitiza kujitolea kwake kwa ushirikiano wa pande nyingi, akihalalisha ushirikiano wa kijeshi na Moscow kwa kutaja matumizi ya kihistoria ya silaha za Urusi na jeshi la Madagascar. Hoja hii imeshindwa kuwashawishi waangalizi, kutokana na idadi inayoongezeka ya vifaa vya Urusi tangu alipochukua madaraka.