
Nchini Senegal, kuitishwa kwa wabunge wawili wa PASTEF na kitengo cha utafiti cha polisi kumezua sintofahamu. Wabunge hao ni Guy Marius Sagna na Cheikh Bara Ndiaye. Kulingana na vyanzo vyetu, watahojiwa kuanzia Juni 1, 2026. Kuitishwa kwao na polisi kunakuja wakati hali ya kisiasa inanendelea kudorora kufuatia hatua ya rais Bassirou Diomaye Faye ya kumuachicha kazi Ousmane Sonko kama waziri mkuu mnamo Mei 22.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Dakar, Pauline Le Troquier
Sababu sahihi za kuitishwa kwa wabunge hao wawili wa PASTEF na polisi hazijafichuliwa. Lakini katika taarifa iliyochapishwa jioni ya Jumapili, Mei 31, chama hicho kilionyesha “ghadhabu yake kubwa” kwa jambo hilo. Pastef ilionya tangu mwanzo: “Tunaonya dhidi ya kutumiwa vibaya kwa vyombo vya sheria (…) kwa madhumuni ya vitisho vya kisiasa.” Kwa upande wa mashirika ya kiraia, Amnesty International Senegal, kupitia mkurugenzi wake Seydi Gassama, ina wasiwasi kuhusu “madai ya ukiukwaji (…) unaohusiana na uhuru wa kujieleza” ambayo, anasema, yanakumbusha yale yaliyotokea miaka ya nyuma.
“Mamia ya mabilioni ya faranga za CFA”
Hati ya kwanza ya polisi inamhusu Cheikh Bara Ndiaye. Siku ya Jumanne, Mei 26, mbunge huyu wa PASTEF aliweza kuepuka jaribio la kukamatwa wakati wa kuapishwa kwa Ousmane Sonko kama Spika wa Bunge la Senegal. Siku mbili mapema, matamshi yake yalizua utata. Kwenye televisheni, alihusisha Waziri wa Fedha na Bajeti, Cheikh Diba, akaunti ya benki ya kibinafsi, ambayo alidai ilikuwa na “mamia ya mabilioni ya faranga za CFA.”
“Wizi katika uchaguzi”
Kesi ya pili inamhusu Guy Marius Sagna, pia mbunge wa PASTEF. Kwenye mitandao ya kijamii, ambapo anaelezea maoni yake mara kwa mara, hivi karibuni alipinga uteuzi wa Waziri Mkuu mpya, Ahmadou Al Aminou Mohamed Lô, akitoa mfano wa utetezi wake wa faranga ya CFA, miongoni mwa mambo mengine. Kwa kumwita mkuu wa nchi “Diomaye mpinzani,” mbunge huyo anadai “wizi katika uchaguzi unaoendelea.” Nchini Senegal, hali ya kisiasa inaendelea kuwa mbaya na isiyo na uhakika wakati raia wanaendelea kusubiri serikali mpya.