Raia wa Ethiopia hivi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu ambao chama tawala cha Waziri mkuu Abiy Ahmed kinatarajiwa kushinda kirahisi kutokana na upinzani kugawanyika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu milioni 50 kati ya raia milioni 130 wa Ethiopia, walijiandikisha kupiga kura kuchagua wawakilishi wao, lakini hali ya utovu wa usalama kwenye maeneo ya Amhara na Oromia, ikitarajiwa kuathiri idadi ya watakaojitokeza kushiriki.

Kwa mujibu wa mfumo wa uchaguzu wa Ethiopia, baada ya raia kuchagua wawakilishi, bunge litapiga kura kumchagua waziri mkuu.

Uchaguzi huu unafanyika wakati ambapo waziri mkuu Ahmed na serikali yake wakituhumiwa kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo kuwanyanyasa wapinzani na waandishi wa habari licha ya ahadi aliyoitoa mwaka 2020.

Aidha kumekuwa na hofu ya kutokea machafuko kaskazini mwa nchi hiyo, hasa baada ya mwezi uliopita, utawala wa zamani wa Tigray, kulirejesha madarakani bunge lililokuwa limevunja kufuatia mkataba wa amani wa mwaka 2022.

Hii itakuwa ni mara ya pili katika kipindi cha miaka 6 kwa eneo la Tigray kutoshiriki kwenue uchaguzi wa kitaifa, hatua inayolinyima eneo hilo haki ya kufanya maamuzi katika bunge la wawakilishi 547.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *