Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamefanya maandamano leo mjini Nairobi wakipinga makubaliiano yaliyofikiwa kati ya serikali ya nchi hiyo na Marekani wa kuanzisha nchini kenya kituo cha kuhifadhi Wamarekani wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

Waandamanaji hao wameema hawataruhusu serikali ya Rais Ruto kuchukua hatua yoyote ya kuanzisha kituo kama hicho. Wameitaka polisi kutilia maanani maslahi ya Kenya kwanza na kufanya kazi kama Wakenya.

Waandamanaji hao pia wamesema ni haki yao ya kidemokrasia kupinga uamuzi wa kuanzishwa kituo cha Marekani cha wagonjwa wa Ebola wa nchi hiyo katika ardhi ya Kenya.

Awali iliripotiwa kuwa, watu wawili wamepigwa risasi na kufariki dunia katika mji wa Nanyuki uliopo katikati ya Kenya, wakati wa maandamano dhidi ya mpango wa Marekani wa kuanzisha kituo cha kuwaweka wagonjwa wa Ebola katika kambi ya kijeshi iliyoko Kaunti ya Laikipia.

Mmoja wa wahanga hao alipigwa risasi katika eneo lililo karibu na Kambi ya Anga ya Laikipia ambapo maandamano yalikuwa yanaendelea na alifariki dunia baada ya kupelekwa hospitalini na mwingine alikuwa tayari ameaga dunia alipofikishwa hospitalini.

Mahakama Kuu ya Kenya imesimamishe mpango wa kuanzisha au kuanza kufanya kazi kituo hicho, hadi pale shauri la kikatiba litakaposikilizwa na kuamuliwa.

Jaji Patricia Nyaundi alitoa maagizo hayo Ijumaa baada ya kundi la kutetea haki kupinga mradi huo, likisema kuwa unazua masuala ya kikatiba na ya maslahi ya umma yanayohitaji mapitio ya kimahakama.

Kituo hicho kilichopendekezwa kimeibua mjadala mkali nchini Kenya, kufuatia taarifa kwamba kitatumika kuwashguhulikia raia wa Marekani wanaoweza kuwa wameathiriwa na Ebola wakati wa mlipuko unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Vilevile kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, kuwa Marekani haitawaruhusu kuingia nchini humo waathirika au washukiwa wa ugonjwa wa Ebola na kwamba watatibiwa katika nchi nyingine imewakasirisha sana Wakenya wanaoona kwamba nchi yao inatumiwa kama jaa la taka na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *